Habari

Bernard Membe “Nimeitwa kwenye kikao cha kamati ndogo ya Udhibiti na Nidhamu Dodoma nitahudhuria mapema bila kukosa”

Bernard Membe "Nimeitwa kwenye kikao cha kamati ndogo ya Udhibiti na Nidhamu Dodoma nitahudhuria mapema bila kukosa"

Waziri wa zamani wa mambo ya nje Bernard Membe amethibitisha kuitwa kwenye kikao cha kamati ndogo ya Udhibiti na Nidhamu huku akithibitisha kuhudhuria ingawa hajaweka wazi ameitwa kwenye kamati hiyo ya chama cha Mapinduzi CCM au ni kamati ipi.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter Membe ameweka ujumbe huo huku akithibitisha kuhudhuria mapema bila kukosa, Pia Membe ameweka wazi kuwa Kikao hicho kinatarajia kufanyika Februari 6, 2020.

Ujumbe huo unasomeka hivi:-

“Hatimaye, jana jioni nimepokea barua ya kuitwa kwenye kikao cha Kamati ndogo ya Udhibiti na Nidhamu Jijini Dodoma. Kikao kitafanyika tarehe 6/02/2020 saa 3 Asubuhi kwenye jengo la White House. Nitahudhuria bila kukosa na bila kuchelewa! Stay tuned!”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents