Habari

Berry Black kutoa bonge la Surprise Bilcanas


MKALI wa muziki wa kizazi kipya kutoka Zanzibar,Mbaraka Abdallah,aka,Berry Black anatarajia kumfanyia Surprise kubwa msanii Berry White katika uzinduzi wa nyimbo yake mpya ya ‘Nyumbani sio safi’.

Mwanamuzki huyo anasema uzinduzi huo utafanyika katika ukumbi wa Bilicanas huku akisema anatarajia kufanya kitu ambacho watu hawatategemea kwa msanii mwenzake ambaye mwanzo walikuwa kundi moja na baadaye kugombana.

Hata hivyo alikataa kusema kitu atakachotaka kukifanya kwakuwa ameshaahidi itakuwa ni cha mshangao kwa wengi wao.

‘Nahitaji kufanya tamasha hilo ambalo kwa mwaka huu kwangu liwe la histori kwakuwa nitafanya kile ambacho watu hawatakitegemea.’

Wasanii hao waliingia kwenye ugomvi mapema baada ya kutoa wimbo wao wa kwanza,’Na wewe’.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents