Burudani

Betrice atumia siku yake ya kuzaliwa kubadili jina

Beatrice_wa_tht

Mwanamuzki kutoka THT Betrice Mathew majuzi tarehe 5 Dec alikuwa anasherekea siku yake ya kuzaliwa kwa mtindo wa kipee kwa kubadili jina lake la kimuziki, na kujiweka jina jipya kabisa. mwanamuziki huyo anasema anafanya hivyo kutokana na kuona jina hilo tayari limeshakuwa na mtu.

Betrice ambaye anatamba na nyimbo ya Mapenzi ya kweli, anasema kwamba amebadili jina ili kupata nafasi nzuri ya kujitanua kimuziki kwakuwa tayari kuna mwanamuziki analitumia jina kama hilo, hivyo aliona ni vizuri kuwa na jina lake mwenyewe. Anasema jina amabalo kwa sasa atakuwa analitumia na ndilo analohitaji watu walitumie kwenye kazi zake za kimuziki, ni Nabisha. anasema Jina Nabisha ndilo atakuwa analitumia zaidi kwenye kazi zake za muziki, hasa atakapotoa nyimbo moja kati ya nyimbo mbili Dunia duara na Kidole gumba.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents