Burudani

Beyonce, Adele waongoza list ya wanawake wanaolipwa mpunga mrefu katika muziki

Jarida la Forbes limemtaja Beyonce kuwa ni mwanamke wa kwanza anayeongozwa kulipwa pesa ndefu ambayo ni dola milioni 105 ikihusisha albamu yake ya ‘Lemanade’ pamoja na Tamasha lake la ‘Formation Tour’ huku nafasi ya pili ikifuatiwa na Adele ambaye ameingiza kiasi cha dola milioni 69 ikiwemo na mauzo ya albamu yake ya ’25’.

Namba tatu imekamatiwa na Taylor Swift ambaye ana mpunga wa kiasi cha dola milioni 44 ikiwemo na mauzo ya albamu yake ya ‘Reputation’, Kisha mwanamama Celine Dion (dola milioni 42 ), Jennifer Lopez (dola milioni 38 ), Dolly Parton (dola milioni 37 ), Rihanna (dola milioni 36 ), Britney Spears (dola milioni 34 ), Katy Perry (dola milioni 33) na Barbra Streisand akishika namba 10 kwa kuwa na dola milioni 30.

Orodha hiyo imehusisha ni pamaoja na malipo ya kodi kuanzia Juni 1, mwaka 2016 hadi Juni 1, 2017. Vile vile taarifa hizi zimehusisha kampuni ya Nielsen SoundScan, Pollstar, pamoja na RIAA. Vile vile orodha hii imezingatia mahojiano na watu wanaohusika katika kiwanda cha burudani.

Muonekano wa orodha hiyo:

1. Beyoncé – $105 million
2. Adele – $69 million
3. Taylor Swift – $44 million
4. Celine Dion – $42 million
5. Jennifer Lopez – $38 million
6. Dolly Parton – $37 million
7. Rihanna – $36 million
8. Britney Spears – $34 million
9. Katy Perry – $33 million
10. Barbra Streisand – $30 million

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents