Burudani

Beyonce amchimba mkwara shabiki aliyempiga kofi la kalio wakati akiimba jukwaani na kumwambia atamtoa nje!

Beyonce aka mama Blue Ivy alijikuta anashindwa kuficha hasira zake jukwaani baada ya shabiki mmoja huko Denmark kuzidiwa na mzuka wa show yake na kumchapa kofi la kalio mrembo huyo mke wa rapper Jay Z.

beyonce on stage

Ni jambo la kawaida mwanamuziki anapokuwa ana perform kujaribu kufanya kila aliwezalo kuzidi kuwapagawisha mashabiki ambao hupiga mayowe kama ishara ya kuenjoy kile kinachofanywa na msanii awapo jukwaani. Moja ya vitu wavifanyavyo wasanii wengi huwa ni kushuka jukwaani na kusogea mpaka eneo walipo mashabiki kwa lengo la kuimba nao huku wakimpa mkono.

Kilichomkuta Bey katika concert yake huko Copenhagen, Denmark usiku wa (May 27), wakati aki perform hit song yake ya ‘Irreplaceable’ ni kwamba aliamua kushuka kwa mashabiki ili kuimba nao, ndipo alipojitokeza shabiki mmoja na kumpiga kofi la kalio mke wa Jay Z (pata picha).

Ghafla Bey alisimama na kuacha kuimba, akaitazama mali ya Jigga iliyoguswa kama iko salama! na kisha kumtazama kwa hasira shabiki huyo aliyejichanganya na umati mkubwa wa mashabiki wengine na kumpa maneno machache ya kumtishia kumwondoa shabiki huyo ukumbini hapo “I will have you escorted out right now, alright?”, na akaendelea na show.

Tazama hapa video ya tukio hilo

http://youtu.be/k57y9EZhG9c

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents