Habari

Video: Beyonce amwimbia marehemu Paul Walker ‘I Will Always Love You’ ya Whitney Houston, wakati wa tamasha lake

Mwimbaji wa R&B kutoka Marekani Beyonce Knowles, ni miongoni mwa watu maarufu walioguswa na kifo cha star wa Fast & Furious marehemu Paul Walker.

Bey n walker

Beyonce alitoa heshima kwa Paul Walker wakati wa show yake iliyofanyika Los Angeles Jumanne usiku (Dec 3), kwa kuimba nyimbo mbili za hisia maalum kama dedication kwa muigizaji huyo aliyefariki kwa ajali mbaya ya gari Jumamosi iliyopita (Nov 30) huko California, Marekani.

Nyimbo mbili alizoimba Beyonce ni pamoja na hit ya marehemu Whitney Houston, ‘I Will Always Love You’, pamoja na single yake ‘Halo’, mbele ya umati mkubwa wa watu waliohudhuria show hiyo akiwemo dada wa Kim Kardashian, Khloe Kardashian.

“I dedicate these songs to Paul Walker,” hayo yalikuwa ni maneno ya Beyonce wakati akimkumbuka Walker katika tamasha hilo.

Mashabiki waliokuwa katika tamasha hilo walielezea hisia zao kupitia twitter kwa kile alichokifanya Queen Bey,
“When @Beyonce sang Whitney Houston I will always love you and dedicated it to Paul walker… I cried. That woman sings like no other (sic)”
Mwingine aliandika,
“Legit crying bc everyone’s singing Halo at the top of their lungs and Beyonce dedicated it to Paul walker (sic)”

Tazama video ya Beyonce wakati akiimba ‘I Will Always Love You’

http://youtu.be/0ueB1zlp-Ps

SOURCE: MIRROR

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents