Burudani

Beyonce, Jay & Blue wapanga kwenye nyumba ya dola 400,000 kwa mwezi!

Sean Carter aka Jay-Z, mke wake mrembo Beyonce Knowles na mtoto wao Blue Ivy Carter wameamua kubadilisha mazingira kwa kupanga kwenye nyumba ya kifahari huko The Hamptons ambapo watakuwa wakilipa dola laki nne kwa mwezi.
Kiasi hicho ni zaidi ya shilingi milioni 630. It’s not a joke!
The Hamptons ni kundi la vijiji na makazi kwenye miji ya Southampton na East Hampton, ambayo huunda tawi la kusini la eneo la Long Island, New York.
The Hamptons inajumuisha makazi aghali zaidi nchini Marekani.
Familia hiyo ya Jay-Z itakaa kwenye nyumba hiyo wote wa August.
Kwa mujibu wa gazeti la The New York Post, wapenzi hao na mtoto wao wa miezi saba wameikodi nyumba hiyo yenye 31,000-square-foot eneo la Bridgehampton ijulikanayo kama Sandcastle.
Nyumba hiyo ya kifahari ipo sokoni na inauzwa dola milioni 43 japo Bey na Jay wanataka kupumzika tu kwenye muda huu wa kiangazi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents