Burudani

Beyoncé, Jay Z, Kendrick Lamar kuhudhuria birthday ya Obama

Beyoncé, Jay Z, Kendrick Lamar watahudhuria sherehe ya siku ya kuzaliwa ya rais wa Marekani, Barack Obama.

obama

Obama atasherehekea kufikisha miaka 55 usiku wa Ijumaa hii kwenye ikulu ya White House na kuhudhuriwa na mastaa kibao.

Mtandao wa Page Six umeripoti kuwa Michelle Obama anaangusha party ya siri ya kukata na shoka kwa Obama kusherehekea birthday yake ya mwisho akiwa kama rais.

Umedai kuwa Usher atatumbuiza kwenye sherehe hizo pamoja na Kendrick Lamar ambaye Obama anamkubali sana. Wageni wengine ni pamoja na Ellen DeGeneres, Sarah Jessica Parker, Stevie Wonder, Jennifer Hudson, John Legend na Magic Johnson.

Wanasiasa watakaokuwepo ni pamoja na mgombea urais mwaka huu wa chama cha Democratic, Hillary Clinton na makamu wa rais, Joe Biden.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents