Bi Nasma Khamisi Kidogo, kumbe bado wamo?
Msanii mkongwe katika muziki wa mwambao nchini Tanzania yaani taarabu Bi Nasma Khamisi Kidogo hivi karibuni ametoka tena na albam yake mpya itakayokwenda kwa jina la dawa ya deni
Msanii mkongwe katika muziki wa mwambao nchini Tanzania yaani taarabu Bi Nasma Khamisi Kidogo hivi karibuni ametoka tena na albam yake mpya itakayokwenda kwa jina la dawa ya deni na pia ameachia ngoma zake mbili ambazo zinatarajiwa kuwa ni tishio katika muziki huo unaoonekana kupanda chati kila kukicha.
Albam ina jumla ya nyimbo sita na imerekodiwa katika studio za sound crafters zilizopo maeneo ya Changombe na hii ikiwa ni albam ya pili kutoka kwa msanii akiwa kama msanii wa kujitegemea.
nazijua nizipendazo ndio jina la albam iliyopita ya msanii huyu mkongwe, ambapo alitamba na vibao kama mahaba ya dhati na tunapendana kwa dhati ambazo mpaka leo bado zinafunika ile mbaya katika medani ya muziki wa taarabu hapa jijini.
japo nazeeka lakini naamini mimi ni msanii na naipenda sana kazi yangu hivyo sichoki kabisa kufikiria mbinu mpya za kuifanya sanaa yangu isizeeke, ndio maana hata katika albam yangu hii mpya nimejaribu kuja tofauti na kwa kufanya nyimbo zenye mahadhi ya zouk, RnB, pia kuna nyimbo nimerap.
Mwanamama huyu amewahi kutamba sana na vibao vyake kama vile mambo iko huku alipokuwa katika kundi lililowahi kujinyakuia umaarufu hapa jiji la Muungano culture troup.
Sikiliza “Sabal Kheri”
{play}nasma_khamis_kidogo_sabal_kheri.mp3{/play}