Tupo Nawe

Bi. Sandrah amkumbuka Zari, “Mwanamke usafi gaga kulisugua”

Stori kubwa kwa sasa ni kuhusu Zari kuonekana kwenye video ya wimbo mpya wa Diamond Iyena – Baadhi ya mashabiki wamefurahia hilo lakini wengine wameonekana kukereka.

Sasa kubwa zaidi Mama mzazi wa Diamond, Bi Sandrah kupitia mtandao wa Instagram ameweka picha ya Zari na kuandika ujumbe wa kumsifia zaidi.

“Mama Latiffah mwenye…#IYENA yake Mwanamke usafi gaga kulisugua Mume akirudi sharti viatu kumvua… @diamondplatnumz ft @rayvanny,” ameandika Bi. Sandra kwenye mtandao huo.

Naye Esma Platnumz amemjibu mama yake kwa kucomment kwenye picha hiyo kwa kuandika, “Heee kwenye USAFI SASA mama TEE NAMPONGEZA wallah dada msafi huyu Kwenye Mapishi @wemasepetu unanikomeshaga.”

Video ya wimbo huo wa Iyena, indaiwa umefanyika kati ya mwezi Juni hadi Sepetemba mwaka jana.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW