Bia yapanda Bei

Kampuni ya Bia Tanzania Ltd (TBL) imepandisha bei ya bidhaa zake kutokana na malighafi zinazotumika katika uzalishaji wa vinywaji hivyo kupanda kwa zaidi ya asilimia 27

Kampuni ya Bia Tanzania Ltd (TBL) imepandisha bei ya bidhaa zake kutokana na malighafi zinazotumika katika uzalishaji wa vinywaji hivyo kupanda kwa zaidi ya asilimia 27.


 


Alisema Mkurugenzi Uhusiano wa kampuni hiyo, Bw. Phocas Laswai, alisema kupanda kwa bei ya bia zinazozalishwa na TBL kunatokana na sababu kuu mbili, kwanza kupanda kwa malighafi zinazotumika katika uzalishaji wa bia na ya pili kukosekana malighafi hizo kwa kiwango kilichokuwa kikipatikana awali.


 


“Bei ya kimea kiungo muhimu katika uzalishaji wa bia imepanda kwa asilimia 27. Kama ingekuwa si kuzingatia ubunifu na uzoefu wa kazi bia moja ingetakiwa iuzwe sh. 2,000 lakini pamoja na kupanda huko kwa gharama za uzalishaji bado tumepandisha sh. 100 tu katika kila chupa moja ya bia. Mwanzo tulikuwa tunaiuza sh. 900 sasa tutauza sh. 1000,” alisema Bw. Laswai



Akielezea sababu nyingine zilizopelekea kupanda kwa bei ya kimea, ni bada ya idadi kubwa ya wakulima kuhama katika kilimo cha shairi na kwenda kulima mahindi na ngano, ukiangalia utagundua kuwa zao hili kwa nchi za magharibi limekuwa na soko sana kwa watengenezaji wa mafuta aina ya petrol.


 


Alisema bei ya kimea duniani iliyokuwa inauzwa pauni 310 kwa tani moja sasa imefikia pauni 632 hadi 710 kwa tani kadirio ambalo ni sawa na ongezeko la mara mbili zaidi ya bei iliyokuwa ikiuzwa awali.


 


“Huko Ulaya wakulima wamekuwa wakiangalia maslahi zaidi. Mfano ambao wakulima wengi waliokuwa wanalima shairi wamegeukia kulima mahindi na ngano kutokana na kuwa mazao hayo yana soko kubwa kwa utengenezaji wa mafuta ya petroli. Hilo likifikia Afrika sijui kama bia itaweza kunyweka kutokana na kupanda kwa gharama yake,”alisema


 


Kutokana na hali hiyo Bw. Laswai alibainisha kuwa mahitaji ya kimea duniani yamekua kwa asilimia 20 na kuongeza kuwa nchi ya China na Urusi ambazo zilikuwa zikitumia vinywaji vya wiski sasa wamegeukia katika kinywaji cha bia, hivyo kusababisha uzalishaji wa kinywaji hicho kuwa na thamani ya juu.


 


“Kiwango cha wanywaji wa bia kimepanda kwa asilimia 20 hasa kwa nchi ambazo awali zilikuwa zikitumia vinywaji vikali kama wiski na vodka sasa wamevamia bia. Kwa hali halisi inavyojionesha katika soko la bia duniani ni kwamba kuna wanywani wengi walioongezeka ghafla ambapo kulingana na malighafi zilizopo itaweza kugharimu miaka miwili kumudu wingi wa wateja waliopo,” alisema


 


Alisema tayari matangazo yatakayo onesha ongezeko la bei kwa kila bia inayozalishwa na kampuni hiyo yameanza kusambazwa katika baa na sehemu zote zenye vibali vya kuendesha biashara ya bia na tamko rasmi kuhusiana na upandaji wa bei ya bidhaa zinazozalishwa na TBL litatolewa kwa vyombo vya habari mwishoni mwa wiki hii.


 


 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents