Tupo Nawe

‘Biashara ya familia inaumiza sana’ – Asema Peter wa P-Square, ataka kaka yao Jude Okoye avuliwe umeneja

Msanii wa kundi maarufu la P-Square, Peter Okoye kutoka Nigeria amethibitisha kuwepo kwa tofauti kati ya ndugu hao na meneja wao ambaye pia ni kaka yao mkubwa Jude Okoye.

P-Square-2014

Siku ya Jumanne (Feb 16) Peter alimwaga mvua ya tweets kueleza kuhusu kutofautiana na meneja wao na kuwatahadharisha watu wasifanye biashara yoyote na kaka yao kwani wao hawataitambua.

jude
Jude Okoye

Jude Okoye amekuwa meneja wa kundi hilo toka lilipoanzishwa.

“Mahabiki wa P-Square najua mmekuwa mkiuliza maswali mengi kuhusu sisi, Sina tatizo lolote na Paul bali ni uongozi.” ilisomeka tweet moja ya Peter.

Katika tweet hizo Peter amesisitiza kuwa hawamtaki kaka yao Jude kuwa meneja tena wa kundi hilo na kuwa wanahitaji kuubadilisha uongozi mzima. Moja ya sababu aliyoitaja ni kutoridhishwa na uongozi huo aliodai unawaongoza bila kuwa na mfumo.

Pacha wa Peter, Paul Okoye na kaka yao mkubwa Jude Okoye hawajasema chochote hadi sasa kuhusiana na tweets za ndugu yao.

Tweet hizo zimesomeka hivi:

“Uaminifu wangu kwa PSquare na mashabiki utaendelea kubaki kwa asilimia 100.”

“Meneja anaajiriwa na msanii na sio kinyume na hivyo.”

“PSquare ni Peter na Paul Okoye.”

“Usher Raymond amewahi kufanya, Beyonce amewahi kufanya pia, hivyo sio kitu kipya.”

“Watu hubadili uongozi na hauna tofauti.”

“Peter na Paul wanahaki ya kuutimua uongozi mzima, biashara ni biashara. Basi.”

“Peter na Paul ni Psquare, na mtu mwingine yeyote ni kiambatanisho tu.”

“Tafadhali yeyote anayefanya malipo na Northside Entertainment au Jude Okoye kwa niaba ya PSquare ajue isi hatuhusiki.#Onyo”

“Biashara ya familia inaumiza sana”.

“Unawezaje kuendesha biashara bila kuwa na mfumo.”

“Nimewahi kujutia vitu vingi kwenye maisha yangu…lakini niamini hili sio moja wapo. #HakunaTenaBiasharaYaFamilia.”

“PSquare haivunjiki. Lakini uongozi lazima uondoke.”

p1

p2

p3

p4

p5

p6

p7

p8

p9

p10

p11

p12

p13

p14

p15

p16

p17

p18

p19

p20

p21

p22

p23

p24

p25

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW