Biashara ya mabinti yaibuka Ukerewe

WAKATI kiwango cha uchumi nchini kikielezwa kukua, imeelezwa kuwa hali za kiuchumi za baadhi ya wananchi wanaoshiriki kukuza uchumi huo zimeendelea kuwa duni

na Sheilla Sezzy


 


WAKATI kiwango cha uchumi nchini kikielezwa kukua, imeelezwa kuwa hali za kiuchumi za baadhi ya wananchi wanaoshiriki kukuza uchumi huo zimeendelea kuwa duni.


Hali hiyo imewafanya watu wengi kukata tamaa na kujiingiza katika biashara haramu ambazo zinakiuka maadili ya Mtanzania.


Hayo yalibainika hivi karibuni wilayani hapa, na mwezeshaji kutoka katika shirika la Kivulini, linalotoa huduma ya kutetea haki za wanawake, Jovitha Mlay, wakati alipokuwa akitoa mada kuhusu maambukizo ya virusi vya ukimwi kwa wanawake.


Washiriki katika mjadala huo, walieleza kuwa baadhi ya kina mama wamefikia hatua ya kuwauza mabinti ili wajipatie kipato.


Akiongea katika mjadala huo, Jesca Mchele, ambaye anajihusisha na biashara ya mama lishe, alisema kuwa imekuwa ni kawaida kwa baadhi ya wanawake ambao wanajihusisha na shughuli za mama lishe na wamiliki wa mabaa katika fukwe, kuajiri wasichana kwa ajili ya kuwasaidia kutoa huduma na wakati huo huo wanawauza kwa wavuvi.


“Hii inaonyesha wazi kuwa hali ya kiuchumi kwa jamii ya wavuvi ni mbaya wakati wavuvi hawa hawa wanachangia kwa kiasi kikubwa kukuza uchumi wa nchi pasi wao kupata manufaa yoyote makubwa, hali inayosababisha wajiingize katika maadili mabaya,” alisema Mchele.


Alisema Wakerewe bado wanaamini kuwa sherehe yoyote ambayo inafanyika bila ya kuwa na mabinti wengi, basi hiyo si sherehe na watu wengi wanaisusia sherehe ya aina hiyo.


Alisema wasichana hao nao wanalazimika kufanya vitendo hivyo kutokana na hali zao mbaya kiuchumi, kwani wanaamini kuwa kujiuza kutawapatia angalau fedha kidogo za kujikimu.


 


 


Source: Tanzania Daima

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents