Burudani

Bibi Cheka kula sahani moja na Wana Hip Hop

Bibi_Cheka_face

Kundi la muziki la mkubwa na Wanawe kila siku limekuwa likikuwa kwa kasi na kuleta vihja na gumzo kwa mashabiki wa kundi hilo kutokana na ukali wa wasanii wake. Kundi hilo baadaya kumtoa msanii mdogo kuliko wote Dogo Aslay huku akijiandaa kuja dogo mwigine zaidi ya Aslay yaani hapa namzungumzia Dogo Muu (Wa pili kushoto toka Saidi Fela na anayefuata  ni Bibi Cheka) , kundi hilo sasa limefanya mabadiliko mapya baada ya kumleta msanii mzee kuliko wote katika muziki wa Bongo Fleva Bibi Cheka anayegonga miaka 51


Bibi Cheka si mgeni katika fani ya muziki, lakini ni mgeni katika uimbaji wa muziki hasa baada ya miaka ya sabini, kuwa miongoni mwa wanamuziki kumi na sita katika kundi la Makocha ambao walikuwa wakinengua na kusasambua kwenye bendi ya Msondo Ngoma kitambo hicho.

Bibi_Cheka

Zaidi na zaidi bibi huyo alikaa na kufikiria hasa baada ya kufikiria kwamba ng’ombe atazeeka lakini maini bado yatakuwa yakijana kwakuwa maini hayazeeti, pia ndipo akajipima na yeye kuona umbo limzeeka lakini sauti na uwezo bado upo na kuamua kurudi tena kwa kasi kwenye idara ya muziki wa kisasa maarufu kama Bongo Fleva, huku akiwapa ahadi kibao mashabiki wake kama atawagongea mpaka Hip Hop, RnB na ngoma za asili pia yumo, ila akasema kwenye taarabu hapo hatogusa kwakuwa hana hulka na nyimbo hizo na kubaki kama shakibi.

Bibi_Cheka_mwenyewe

Hivi sasa mwanamziki huyo ameshakamilisha wimbo wake wa Ni wewe katika sttudio ya Poteza Record chini ya Producer Mr India Suresh, na hivi sasa kuanzia kesho anaanza kushoot video ya wimbo huo, ili mtakapokuwa mnamsikiliza pia mumuone kwenye kitu cha Chupa…

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents