Burudani ya Michezo Live

Bibi wa Miaka 62 asimulia alivyotongozwa na kuolewa na kijana wa miaka 24 “Ananipa mambo matamu sijawahi kupata popote” – Video

Bibi wa Miaka 62 asimulia alivyotongozwa na kuolewa na kijana wa miaka 24 "Ananipa mambo matamu sijawahi kupata popote" - Video

Ndoa iliyoleta maneno mengi sana mitandaoni ni hii inayowahu watu wawili ambao wamepisha miaka takribani 38 lakini hawakuangalia hicho wao waliangalia upendo.

Innocent Nyange na Gokeys Dokeys ni wanandoa walifunga ndoa mwaka 2019 mwezi wa kumi na wamezua gumzo kutokana na umri wao ambapo mama aliyeolewa anaumri wa miaka 62 ambao ni mara mbili ya umri wa kijana aliyemuoa mwenye umri wa miaka 24 tu huku ukiwa ni umri mdogo kuliko mtoto wa kwanza wa huyo mama mwenye miaka 30 wa kiume ingawa ana watoto wawili tu, huyo wa kwanza wa kiume mwenye umri wa miaka 30 lakini mwigine wa kike.

Akiongea Innocent amesema kuwa mtoto wa bibi huyu mwenye umri wa miaka 30 ndio anayemsapoti sana kwenye mahusiano yake na mama yake na mara nyingine hushauriana mambo ya kimaisha. Hata hivyo Innocent amedai hajampendea Gokeys kwa sababu ya hela kwani hana hela kama watu wanavyofikiria.

Akiwa kama msanii Gokeys Dokeys ameeleza nia yake ya kufanya kazio na wasanii wa Bongo Fleva na kusema kwamba yeye anawafahamu baadhi ya wasanii wa Bongo Fleva hasa Rayvanny na Darrasa ila msanii kama Diamond na Alikiba hajui nyimbo zao.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW