Siasa

Biden aomba msamaha kwasababu ya wanajeshi kulala eneo la kuegesha magari

Rais Joe Biden wa Marekani ameomba msamaha baada ya baadhi ya wanajeshi waliokuwa wamewekwa kulinda eneo la Capitol kupigwa picha wakiwa wamelala katika eneo la kuegesha magari.

Zaidi ya wanajeshi 25,000 walipelekwa Washington DC kwa ajili ya kushughuli ya kuapishwa kwake mapema mwezi huu.

Picha walizopigwa maafisa hao zilianza kusambaa mtandaoni Alhamisi zikiwaonesha wakiwa wamepumzika katika eneo la karibu la kuegesha magari wabunge waliporejea.

Hali hiyo ilisababisha hasira miongoni mwa wanasiasa huku baadhi ya magavana wakawaondoa wanajeshi wao kwasababu ya utata huo.

Bwana Biden alizungumza na mkuu wa jeshi la kulinda usalama wa taifa Ijumaa, kuomba msamaha na kuuliza ni kipi ambacho kingekuwa kimefanywa kuweka mambo sawa, kulingana na vyombo vya habari vya Marekani.

Mama wa taifa Jill Biden pia naye alitembelea baadhi ya vikosi hivyo kuwashukuru akiwa amewabeba biskuti kutoka Ikulu kama zawadi.

“Leo hii nilitaka tu kuja na kuwashukuru kwa kutulinda mimi pamoja na familia yangu,” alisema.

 

Picha hizo zinazoonesha mamia ya wanajeshi wakiwa eneo la kuegesha magari zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii Alhamisi na kusababisha hasira.

U.S. first lady Jill Biden surprises National Guard members outside the Capitol with chocolate chip cookies
Maelezo ya picha,Mama wa taifa aliwatembelea baadhi yao baada ya kutokea kwa utata huo

Wengi walianza kuzungumzia juu ya hali hiyo huku wanajeshi hao wakiwa wanapigwa na moshi wa magari wakiwa hawana uwezo wa kufikia maeneo muhimu kama choo baada ya kuwa katika hali ya tahadhari kwa siku kadhaa.

Kuna taarifa za kukanganya kuhusu kwanini wanajeshi hao walipelekwa Capitol lakini vikosi kadhaa walielezea vyombo vya habari kwamba agizo hilo liliwafikia Alhamisi mchana bila maelezo yoyote.

Picha hizo pia zimesababisha wasiwasi juu ya kusambaa kwa virusi vya corona miongoni mwa wanajeshi hao.

Afisa wa Marekani ambaye hakutaka kutambuliwa aliyezungumza na shirika la habari la Reuters Ijumaa, amesema kwamba kati ya wanajeshi 100 na 200 ya waliopelekwa eneo hilo walikuwa na virusi vya corona.

Baada ya picha hizo kuanza kusambaa, wabunge walionesha hasira zao kwenye mitandao ya kijamii huku wengine wakitoa ofisi zao kama sehemu ambazo wanaweza kupumzika.

Ruka Twitter ujumbe, 1

Mwisho wa Twitter ujumbe, 1

Presentational white space
Ruka Twitter ujumbe, 2

Mwisho wa Twitter ujumbe, 2

Presentational white space

Baadaye Alhamisi ilisemekana kuwa uamuzi huo umebatilishwa pale wanajeshi hao waliporuhusiwa kurejea Capitol.

Gavana wa jimbo la Florida, Ron DeSantis, alikuwa miongoni mwa wale waliosema kuwa ametoa agizo wanajeshi wa jimbo lake kurejea nyumbani kufuatia mtafaruku huo.

Chuck Schumer, mbunge wa Democrat na kiongozi mpya wa Bunge la Seneti, alisema kilichotokea ni “jambo baya” na kuahidi kuwa “halitarejelewa tena”Kamati ya kanuni za bunge la Seneti pia inachunguza suala hilo, Seneta Roy Blunt amezungumza na shirika la habari la Politico.

Taarifa ya pamoja kutoka kwa kikosi cha ulinzi wa taifa Marekani na maafisa wa polisi wa Capitol, Ijumaa wamesema wameshirikiana kuhakikisha waliopelekwa eneo la Capitol wanamazingira mazuri yanayowawezesha kutekeleza majukumu yao.

Pia waliongezea kuwa wanajeshi ambao hawako kazini, wamepewa makazi katika mahoteli na maeneo mengine na kuwashukuru wabunge kwa kuangazia suala hilo.

Baadhi ya maafisa 19,000 wa ulinzi wa taifa watarejea makwao katika siku zijazo huku wengine takriban 7,000 wakitarajiwa kuwa Washington, kulingana na gazeti la New York Times.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents