Burudani

Bifu ni kama sheria – Madee

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Madee amekiri kuwa kwenye muziki hata iweje bifu ni lazima zitatokea hii ni kutokana na wasanii kufanya kitu cha aina moja huku akidai kuwa kitendo hicho kinachangamsha muziki.

Tokeo la picha la madee
Madee

Madee amesema bifu lazima ziwepo ili kuchangamsha muziki kwani muda mwingine zinaweza zikatumika kibiashara ili mradi kusiwe na chuki kutoka moyoni au zile bifu za kushikiana mapanga au kutukanana mitandaoni.

“Wanamuziki na bifu ni kama sheria ipo hiyo …kwa sababu tunafanya biashara moja lazima tunatengezeana chuki fulani..na ambao wana publish vitu hivyo vinakuwa vikubwa ni wananchi kwa sababu hawajui kwamba fulani na fulani wanafanya hivyo kwa sababu ya nini? Muda mwingine bifu inachangamsha gemu na muda mwingine ni biashara”,amesema Madee kwenye mahojiano yake na Gazeti la Mwananchi.

Kwa upande mwingine Madee amesema bifu ni nzuri ila isifikie mahala wahusika wakaanza kutukanana mitandaoni au kutafutana mitaani kwa mapanga kwani hiyo inakuwa ni vita na sio bifu tena.

SOMA ZAIDI: Nay wa Mitego aijibu diss ya Madee kwenye ‘Hela’, auita wimbo mbaya kuliko mbaya za mwaka huu

Madee kwa miaka ya hivi karibuni amekuwa na bifu na wasanii wenzake kama Ney wa Mitego na Afande Selle ambapo mpaka leo bado tofauti hizo hajatamka wazi kama alishazipotezea.

By Godfrey Mgallah

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents