Burudani

Bifu nyingine?!

TID amedai kwamba Hasheem Thabeet amempiga usiku wa Jumamosi iliopita katika ukumbi wa Bilicanas, hayo yameandikwa katika blog yake:

“Ilikua majira ya saa kumi unusu nikiwa natoka club billcanas pamoja na rafiki yangu ANNA tukiongozana kuelekea mlango mkubwa wa kioo nikiwa naongea na simu na Hisbert kwa sauti ya juu maana kelele za muziki zilikua zinasumbua nikiwa nimesimama nje ya mlango wa kioo ghafla akatokea bwana HASHIM ambaye alikua counter akiongea na wakata ticket akaja nje na kunipiga bonge la mtama nikaaunga chini ya sakafu na kuzirai kwa dakika kadhaa,mabaunsa wakanibeba na kuniweka pembeni maana nilikua mlangoni,nilipozinduka nilisikia maumivu makali kwenye mabega,mkono wangu wa kulia na mguu ambao unafanya kutembea kwangu kwa taabu,nikaangalia mkononi simu yangu sikuiona tena,nikawauliza mabaunsa wake jamaa amekwenda wapi!wakadai ameondoka tayari…nikajikokota kuelekea kwenye gari yangu na kuelekea polisi kutoa taarifa niweze kupata matibabu,nilipofika nikaaandika statement nikapewa namba ya case CD/RB/6848/10 pia nikapatiwa PF3 nikaenda hospitali nikapata matibabu,sasa hivi niko kitandani siwezi kutembea vizuri,pia nitashindwa kuperfom kwenye harusi ambayo tayari nishalipwa pesa tayari.SWALI langu ni kwanini ameamua kunidhalilisha vile mbele ya CLUB na FANZ ambao nilikua nawatumbuiza?kwanini ameamua kuniharibia kazi yangu?kwanini ameamua kunipiga bila ya kumkosea?JE NI SAWA HIVI JAMANI….naona  MACHOZI YANANITOKA SINA CHA KUMUELEZA MAMA YANGU.” TID

Wadau tunaendelea kuwatafuta mastaa wetu ili kujua ukweli wa hili jambo. Kama kuna mwenye habari zaidi awasiliane nasi.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents