Habari

Big Brother Africa: Kenya na Uganda zaanza vibaya, Huddah na Denzel wauaga mchezo

Hakika usiku wa jana Jumapili (June 2) haukuwa mzuri kwa wana Africa Mashariki hususani nchi za Kenya na Uganda baada ya team zinazowawakilisha katika Big Brother “The Chase” kupungua nguvu kutokana na wawakilishi Huddah Manroe wa Kenya na Denzel wa Uganda kupewa tiketi za kurejea makwao.

Denzel & Huddah2

Mishale ya saa 1 za usiku kwa saa za Afrika Mashariki macho ya watazamaji wa nchi mbalimbali za Africa yalielekezwa katika Eviction show ya kwanza ya Big Brother Africa “The Chase” ambayo ndio ilikuwa na majibu ya nani watakaopewa tiketi za kurudi nyumbani usiku huo baada ya kudumu kwa wiki moja tu toka shindano hilo lianze wiki iliyopita (May 26).

Washiriki watano waliokuwa kikaangoni ni Huddah, Denzel, Selly, Natasha pamoja na Betty na kura za watazamaji zilifanikiwa kuwaokoa Selly, Natasha na Betty na kuwaacha Huddah na Denzel warudi nyumbani kuendelea na maisha yao ya kawaida.

Muda mfupi baada ya Huddah na Denzel kujua hatma ya uwepo wao katika jumba hilo lenye raha ya kila aina, Huddah ali tweet kwa mara ya kwanza toka tweet yake ya mwisho ya (June 19), na tweet yake ya kwanza jana ilikuwa “‏@HUDDAHMONROE.. And such is life….back to the hustle!” , iliyofuatiwa na tweet nyingine ya kuwashukuru fans wake wa Kenya na Africa kwa ujumla ‏”Thanks alot Kenya and the whole of Africa….You did ur part.God bless”.

Hivi ndivyo kura zilivyopigwa na kuamua nani atoke na nani abaki kati ya washiriki watano waliokuwa wako kwenye kikaango cha eviction:

votes

Hapo chini utaona ni nchi gani ilimpigia kura mwakilishi gani aliyekuwa kwenye kikaango cha eviction.

Angola: Betty
Botswana: Betty
Ghana: Selly
Kenya: Huddah
Ethiopia: Betty
Malawi: Natasha
Namibia: Betty
Nigeria: Selly
South Africa: Denzel
Sierra Leone: Betty
Tanzania: Huddah
Uganda: Denzel
Zambia: Natasha
Zimbabwe: Natasha
Rest of Africa: Selly

Jumla: Betty = 5; Selly = 3; Natasha =3, Denzel = 2, Huddah = 2. (Total: 15 Votes)

Kwa mujibu wa kura za watazamaji kura za Huddah na Denzel ndio zilizokuwa ndogo na hivyo kuwafanya washindwe kuendelea na shindano ambalo hata hivyo siku ya 91 ikifika ni lazima apatikane mmoja tu atakaeondoka na kitita cha $300,000.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents