Burudani

Big Brother Africa Updates: Wawakilishi wa Kenya, Angola, Malawi na Zimbabwe wamekuwa nominated kutoka wiki hii!

Linapokuja swala la nomination za nani atoke katika mchezo ndipo ‘umimi’ unapochukua nafasi sababu kila mmoja alijaza fomu za kushiriki kwa lengo la kushinda $300,000 za Big Brother ‘The Chase’ na mshindi ni mmoja tu.

the chase

Ikiwa ni wiki ya tatu ya shindano linalowaunganisha waafrica kifikra kwa siku 91, tayari majina ya washiriki wa Ruby na Diamond house walio hatarini kutoka wiki hii yameshafahamika.

Angola ndio ambayo inapumulia mashine safari hii sababu washiriki wote wawili Biguesas na Neyll wamependekezwa kuchapa lapa. Nchi nyingine ambayo hata haijapumua baada ya mshiriki wake kuliaga shindano wiki ya kwanza ni Kenya, ambayo mshiriki wake Annabel ameingia katika kikaango cha biggie.

Biguesaas
Biguesas (Angola)

Neyll
Neyll (Angola)

Annabel
Annabel (Kenya)

Washiriki wengine walioingia danger zone ni Natasha wa Malawi na Pokello wa Zimbabwe.

Natasha bb
Natasha (Malawi)
Pokello zimbabwe
Pokello (Zimbabwe)

Katika orodha ya wiki hii Bolt wa Sierra Leone amepona kwa mara ya pili, wiki iliyopita alipendekezwa kutoka lakini aliokolewa na kipenzi chake Betty aliyekuwa HOH, na wiki hii amependekezwa kwa kura nyingi lakini ameokolewa tena na HOH wa Diamond Melvinopted na nafasi yake kupewa Annabel.

Je unadhani Bolt anaweza kukwepa ‘risasi’ za kutolewa mpaka lini? Yawezekana ameingia mjengoni na bulletproof ya ‘babu’ LOL!

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents