Habari

Big Brother Africa: Washiriki watano waingia danger zone, wawili kutoka Jumapili hii

Ni wazi kwamba washiriki wote wameingia katika Big Brother wakijua kuna kutoka na kushinda, japo ni jambo gumu sana kwa mshiriki atakayechaguliwa kutoka baada ya wiki moja tu.

bba housemates

Baada ya saa 24 kupita toka mchezo uanze big brother alitoa tangazo la washiriki watano walioingia katika hatari ya kuiaga Big Brother “The Chase” Jumapili hii (June 2).

Majina ya washiriki walio katika hatari ya kutoka ni matano lakini watakaofungasha mizigo yao Jumapili hii ni wawili kati yao.

Upande wa Rubies House walio katika list hiyo ni hawa:

selly
Selly wa Ghana

natasha bba
Natasha kutoka Malawi.

Upande wa Diamond House panga la eviction limemdondokea Betty wa Ethiopia baada ya mkuu wa nyumba hiyo Fezza kumuokoa mshiriki wa Ghana Elikem ambaye ndio aliyekuwa amechaguliwa na Big Brother.

betty
Betty wa Ethiopia

Moja ya mamlaka aliyonayo mkuu wa nyumba ni pamoja na kumuokoa mshiriki anayekuwa amechaguliwa kutoka, kwa kumpendekeza mshiriki mwingine kwa niaba yake.

Washiriki wengine waliongia katika hatari ya kutoka weekend hii ni muwakilishi wa Kenya Huddah Manroe, pamoja na Denzel kutoka Uganda.

Huddahbbacover
Huddah Manroe

DENZEL
Denzel

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents