Michezo

Bila Andy Murray mchezo wa tennis hauna mvuto – Becker

Gwiji wa mchezo wa tennis na aliyejizolea mafanikio makubwa, Boris Becker amesema kuwa katika mchezo huo pasipo Andy Murray hakuna mvuto.

Mchezaji tennis, Andy Murray akiwa katika michuano ya Wimbledon mwaka jana

Becker amesema kuwa mchezo wa tennis unamuhitaji Andy Murray ili kuwa na mvuto na ushindani wakipekee.

Gwiji wa mchezo huo, Boris Becker akiwa katika tuzo za michezo za dunia 

Murray anatarajiwa kurejea tena kunako viunga hivyo baada kuuguza majeraha yake tangu mwaka jana katika robo fainali ya michuano ya Wimbledon.

Bingwa huyo mara tatu wa Grand Slam, Murray amesema anatumaini atarejea tena katika mashindano kipindi cha majira ya joto ndipo gwiji wa mchezo huo, Becker akiamini kuwa hayo ni maamuzi mazuri na wapenzi wa tennis wasubiri kuona ushindani tena ukirejea katika viwanja mbalimbali.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents