Tragedy

Bilionea auawa kikatili Moshi, apigwa risasi 20, alikuwa anaongoza kwa utajiri Mererani

Mfanyabiashara tajiri wa Mirerani na Jijini Arusha, Erasto Msuya, ameuawa kwa kupigwa risasi zaidi ya 20 kwa kutumia bunduki aina ya Sub Machine Gun (SMG), jana mchana.

auawa
Askari polisi wa Wilaya ya Hai wakianda mwili wa mfanyabiashara wa madini Erasito Msuya aliyeuawa kwa kupigwa risasi katika eneo la Wasomali, mkoani Kilimanjaro, kwa ajili ya kuupeleka chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospiotali ya wilaya hiyo. Picha na Dionis Nyato

Erasto anayemiliki vitega uchumi kadhaa na anayeaminika kuwa miongoni mwa wafanyabiashara wa Mirerani wanaoongoza kwa utajiri, aliuawa jana saa 7:00 mchana wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.

“Eneo la tukio kumeokotwa maganda karibu 21 ya risasi zinazoaminika ni za SMG, yaani mwili ni matobo kila sehemu kwa kweli ameuawa kinyama sana,” alisema polisi mmoja wa Kituo cha Bomang’ombe.

Kufuatia mauaji hayo yaliyotokea kati ya neo la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia) na mji wa Bomang’ombe, mji huo ulifurika magari ya wachimbaji kutoka Moshi, Arusha na Mererani.

Habari za uhakika zilieleza kuwa wauaji wake walikuwa katika pikipiki na baada ya kumminia risasi hizo, walimpora kibegi ambacho haikujulikana kama kilikuwa na madini ama mamilioni ya fedha.

Kulingana na vyanzo vya habari, mfanyabiashara huyo alipigiwa simu na kukubaliana kukutana katikati ya mji wa Bomang’ombe na makutano ya Barabara ya Kia katika Barabara Kuu ya Hai kwenda Arusha.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz alisema kuwa mfanyabiashara huyo aliuawa saa 7:00 mchana eneo la Mjohoroni kati ya mji wa Bomang’ombe na makutano ya barabara ya Kia.

“Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa Eransto alikuwa akitokea Moshi kuelekea Arusha, na alipofika hilo eneo la Mjohoroni alichepuka na kwenda meta 300 nje ya barabara,” alisema.

Kamanda Boaz alisema alipofika eneo hilo, alikutana na vijana wawili waliokuwa na pikipiki ambao waliingia ndani ya gari kwa lengo la kufanya mazungumzo yanayodhaniwa ni ya kibiashara.

Hata hivyo, muda mfupi tu Erasto alishuka kwenye gari lake na kuanza kukimbia na ndipo mmoja kati ya wale vijana alishuka kwenye gari la Erasto na kuanza kumminia risasi nyingi.

Source: Mwananchi. Isome habari hii zaidi hapa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents