Habari

Bilionea Mo Dewji bado hajapatikana, Baba yake aulizwa ishu ya simu ya mwanaye kuwa hewani

Jeshi la Polisi bado linaendelea kumsaka mfanyabiashara mkubwa nchini Tanzania Mohamed Dewji ‘Mo’ ikiwa ni zaidi ya saa 48 zimepita tangu atekwe nyara na watu wasiojulikana wakati akingia kufanya mazoezi katika gym ya Colosseum, Oysterbay jijini Dar leo Oktoba 11.

Hadi sasa mamlaka zinazohusika hazijatoa taarifa mpya kuhusu upatikanaji wa ‘Mo’.

Ijumaa hii baba wa mfanyabiashara huyo, Gulam Dewji Hussein alipotafutwa na Mwananchi kuzungumzia taarifa zozote kuhusu mwanaye, alisema familia ilikuwa haijapata chochote kutoka polisi hadi jana jioni.

Alipoulizwa kuhusu simu ya mwanaye inayosemekana ikipigwa inaita na kupokea ujumbe mfupi wa maandishi (sms), mzazi huyo alimtaka mwandishi wa habari hizi asubiri kwa kuwa muda huo (wa jioni) alikuwa na wageni na asingeweza kuzungumzia suala hilo. Hata alipotafutwa baadaye hakuweza kupatikana.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents