Habari

Bilionea Mtanzania Mendes aliyeuza mfumo wake wa kununua gesi kadiri unavyotumia afunguka “Watu waliona nimechanganyikiwa ” (Video)

Bilionea Mtanzania Andron Mendes ambaye aliuza mfumo wake wa kununua gesi kadiri unavyotumia kupitia kampuni yake ya Kopa Ges kwa kampuni ya Cycle Ges ya Uingereza, amefunguka kuzungumzia jinsi alivyoutengeza mfumo huo na namna alivyouuza kwa mabilioni.

“Mwaka 2016 nilikuwa nafanya project ya ujenzi, kwahiyo mambo ya hela yalikuwa ni magumu sana, sasa siku moja niliishiwa fedha kabisa na bahati mbaya na mtungi wangu wa gesi ulikuwa umeisha, na kipindi hicho nilikuwa Mhasibu kwenye kampuni moja ya bima Dar Es salaam. Nikijiangalia mimi nilikuwa chini ya CEO halafu nimefulia sina pesa ya kujaza mtungi wa gesi, sasa lile jambo lilinifanya nianze kutafuta njia ya kukabiliana na tatizo kama hilo, so kesho yake nilivyowauliza wafanyakazi wakasema ni kweli mara nyingi gesi ikiisha kabla haujalipwa mshahara utasubiri mpaka mshahara utoke,” alisema Mendes ambaye kwa sasa amefungua kampuni kubwa na kuajiri watu wengi.

 

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents