Michezo

Bilionea wa Nigeria Aliko Dangote bado anataka kuinunua timu ya Arsenal!

Tajiri wa kwanza Afrika, Aliko Dangote, amekiri kuwa bado ana mpango wa kuinunua club ya Arsenal licha ya kushindwa kufanya hivyo mwaka 2010.

Dangote-OnoBello

Dangote mwenye utajiri wa dola bilioni 15.7 (£10.38bn) anawazidi walimiki wa sasa wa club hiyo, Stan Kroenke (£3.7bn) na Alisher Usmanov (£9.65bn).

“Bado nina matumaini, siku moja kwa bei sahihi kwamba nitainunua timu hiyo,” Dangote aliiambia Bloomberg. “Ninaweza kuinunua, si kwa bei ya kijinga lakini kwa bei ambayo wamiliki hawatataka kukataa. Ninajua mbinu zangu.”

Kwa sasa Arsenal ina thamani £1bn, £988m.

Kama deal hiyo ikifanikiwa, Dangote atakuwa mwaafrika wa kwanza kuwa mmiliki wa timu inayocheza ligi kuu ya England.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents