Habari

Bilioni 10 za Rais Magufuli kuanza kujenga ofisi za idara ya uhamiaji Dodoma (+video)

Waziri wa Mambo ya Ndani, Dkt. Mwigulu Nchemba ametembelea eneo la Mtaa wa NCC lililopo Manispaa ya Dodoma mjini, mkoani humo ambapo ndipo zitajengwa Ofisi za makao makuu ya Idara ya uhamiaji.

Tayari Rais Magufuli, ameshatoa kwa idara hiyo Sh. bilioni 10 na kwamba ujenzi wa ofisi hizo unatarajiwa kuanza hivi karibuni.

Akizungumza wakati alipotembelea ofisi hizo leo, Dk Mwigulu amemshukuru Mheshimiwa Rais, kwa kuwapa fedha hizo ambzo ni Sh bilioni 10 kwa ajili ya ujenzi makao makuu ya Uhamiaji.

Amesema tayari kwasasa eneo kubwa lenye mita za mraba 9,777 limepatikana kwa ajili ya kujenga jengo kubwa na la kisasa kwa idara hiyo.

“Eneo limeshapatika kubwa la kutosha la kujenga ofisi ya kisasa kama ambavyo muheshimiwa Rais amesemea wakati anatuhaidi kutupa fedha hizi sasa tumepata eneo la kutosha ambalo lipo karibu na ofisi zote muhimu kama vitambulisho vya Taifa,zimamoto na ofisi zingine za serikali ambapo itasaidia kama mtu akifika uhamiaji anaweza kupata zingine ambazo zipo karibu,” Aliongeza waziri mwigulu.

Waziri mwigulu ametoa rai kwa idara ya uhamiaji kuendelea kuchapa kazi kwa bidii kwani kuchapa kazi kwao ndio kumefanya wao kupata fedha hizo za ujenzi kwa haraka na fedha za kununua nyumba za makazi ya askari Dodoma kwani kama wangefata kupata fedha katika bajeti ya wizara ingechukua mda mrefu kupatikana fedha hizo hivyo kufanya kazi kwao vizuri kunamfanya hata yeye kuwa waziri wa mamboya ndani mzuri.

Naye, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala amemshukuru muheshimiwa Rais Magufuli kwa kuwapa fedha hizo kujenga jengo la kisasa na mpaka sasa wameshapa eneo kubwa kabisa ambalo litawawezesha kupata mahitaji yote.

“Sisi kama idara tunajukumu la kufuata taratibu zote kwa haraka iwezekanavyo ili jengo hili ndani ya mwaka wa fedha ujao liweze kukamilika kwasababu kama fedha zipo,”alisema Dkt. Anna.​

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents