Habari

Bilioni 10 zatengwa kuboresha daftari la wapiga kura – NEC

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeanza maandalizi ya kufanya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa mwaka wa fedha wa 2017/2018, baada ya Serikali kutenga Shilingi Bilioni 10 kwa ajili ya kazi hiyo.

Hayo yamezungumzwa na Mkurugenzi wa Tume hiyo, Ramadhani Kailima kwa nyakati tofauti wakati akitoa elimu ya mpiga kura katika kituo cha Dodoma FM, kilichopo mkoani Dodoma.

“Tume imeanza maandalizi ya kufanya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura, Serikali imeshatenga Shilingi Bilioni 10 kwa ajili ya kuboresha daftari la kudumu la wapiga kura mwaka 2017/2018.”alisema Kailima.

Aliongeza kuwa kwa kipindi hicho Tume itatoa kadi mpya ya mpiga kura kwa watakaoandikishwa upya, waliopoteza kadi na kadi zilizoharibika, kwa wanaohamisha taarifa zao ikiwemo waliohamia Dodoma, na kufuta wapiga kura waliopoteza sifa za kuwa wapiga kura.

Aidha Kailimia alisema kuwa maandalizi ya uboreshaji huo ni pamoja na kutoa elimu ya mpiga kura kupitia vituo vya redio nchi nzima mpango ambao umeanza kutekelezwa kwa baadhi ya mikoa nchini.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents