Burudani

Bill Nass atoa saluti kwa Madirector wa video Bongo

Msanii wa muziki wa hip hop Bongo, Bill Nass amesema kiwango cha madirector wa video za muziki Bongo kinaridhisha.

Rapper huyo ambaye anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Sina Jambo’ ambayo alishoot nchini Afrika Kusini amesema kutokana na hilo wasanii wengi wamepunguza kwenda nje ya nchi kwa ajili ya kufanya video.

“Wasanii wengi wameacha kufanya kazi nje ni kwa sababu madirector wa nyumbani wanafanya vitu bora zaidi, ndio maana hata mimi nimefanya nje lakini nimefanya na director wa nyumbani,”  Bill Nass ameiambia Bongo5.

“Kuna mazingira yalinilzimu kushoot video kule lakini madirector wetu wanashoot video kali kuliko wote Afrika,” ameongeza.

Katika hatua nyingine ameeleza juu ya kundi la vijana ambao wanaonekana katika video yake hiyo, kwa kusema kuna baadhi ya Watanzania,Waganda na wengine kutoka mataifa mbali mbali ya ukanda wa Afrika Mashariki.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents