Burudani

Bill Nass: Sio kweli kwamba nampa stress Godzilla

Msanii wa Bongo Flava, Bill Nass amesema hana tatizo na Godzilla, na yeye kutajwa kuwa anampa stress Godzilla ni kitu ambacho hakubaliani nacho wala hakipendi.

Rapper huyo ameeleza hayo kupitia XXL ya Clouds Fm, na kubainisha kuwa mtu anaposema Godzilla ana stress anayoisababisha yeye haimletei picha nzuri kwa mashabiki wa pande zote mbili na pia inatengeneza uadui wa moja kwa moja usiokuwa na msingi.

“Inatengeneza picha mbaya kwangu wakati sina tatizo naye, watu wanatakiwa wafahamu sina tatizo na Godzilla na kuja kwangu kwenye muziki sikuja kwa ajili ya mtu mwingine wala mimi sio msanii ambaye nimetengezwa, watu wataelewa hiyo miaka 10 mbele ama sita kwa sababu bado nina muda mwingi wa kufanya muziki,” amesema Bill Nass.

Bill Nass amekuwa akihusishwa na kupotea kwa Godzilla kimuziki kutoka style wanazofanya kushabiana, pia rapper Wakazi aliweka wazi hilo katika diss track ‘‘Zillnass Zillnass’ ’ aliyoiachia kwa ajili Godzilla.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents