Burudani

Bill Nass, TID ‘dude’ kuamshwa muda wowote

Msanii wa muziki wa hip hop Bongo, Bill Nass amedai kuwa kwa sasa ana maelewano mazuri na TID na kuna ngoma wameshafanya.

Wawili hao ambao walitoa hit kama Raha na Ligi Ndogo waliripotiwa kutokuelena baada ya Bill Nass kuhama menejimenti. Hata hivyo rapper huyo anaeleza kuwa baada ya kumaliza tofauti zao kiu yake ni kuja kufanya kazi tena na TID.

“Juzi tu nilikuwa naye Mnyama, ni kaka yangu na ninamuheshimu sometime unajua yanatokea mapishano ya hapa na pale lakini bado heshima yangu kwake ipo pale pale,” Bill Nass ameiambia Bongo5.

“Ninatamani siku moja tufanye kitu kingine, kuna kazi uyyake tulifanya kwa Lamar lakini natamani kufanya naye tena wimbo wangu, hivyo ndivyo muziki unavyotaka,” ameongeza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents