Burudani

Billnass asita kuachia wimbo mpya 

By  | 

Mkali wa wimbo Mazoea, Billnass amedai kwa sasa anashindwa kuachia wimbo mpya kutokana na kukosa muda wa kuisimamia project hiyo.

Rapa Billnass

Rapa huyo ambaye ni mwanafunzi wa chuo cha IFM, ameiambia Bongo5 kuwa  kwa kipindi hiki atakuwa busy na masomo kwaajili ya kujiandaa na mitihani ya mwisho, mwezi September mwaka huu.

“Kazi mpya zinakuja lakini bado kidogo kwa sasa hivi kuna mambo ya chuo yameingilia kwahiyo nashindwa kuachia wimbo mpya kwa sababu nitashindwa kuisimamia,” alisema Billnass.

Aliongeza, “Unajua muziki wa sasa umebadilika sana, huwezi kutoka ngoma ukaiacha bila kufanya promotion yoyote itakuwa ni kazi bure. Unatakiwa ukiachia ngoma uwe tayari kwaajili ya kuzunguka kwenye vituo mbalimbali vya redio na runinga kwaajili ya interview,”

Katika hatua nyingine rapa huyo amewashukuru mashabiki wake kwa ushirikiano waliompatia katika project zake huku akiwaahidi kazi nzuri zaidi.

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments