Burudani

Bilnass amvaa Nay wa Mitego kumtaja kwenye nyimbo zake ‘Nikitaja majina 10, Yeye hayupo’ (+Video)’ (+Video)

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Bilnass amesema kuwa anashangazwa na kitendo cha msanii mwenzie Nay wa Mitego kumtaja taja kwenye nyimbo zake jambo ambalo kwa upande wake ameona halina umuhimu kwani kuna vitu vingi vya msingi vya kuimba.

Akiongea na Bongo5, Bilnass amesema kuwa yeye ni biashara na ndio maana Nay amekuwa akimtaja taja kwenye nyimbo zake ili zitembee ila yeye hawezi kutaja jina la mtu yeyote kwenye nyimbo zake.

Nimegundundua kuwa Tweet yangu ni kubwa kuliko wimbo wake, Na sidhani kama huo wimbo unaukumbuka hadi leo. Kwa hiyo nikagundua kutupa mawe juu ya mayai ni kosa kubwa sana, Kwanini utumie nguvu kubwa kulibeba karatasi,” ameeleza Bilnas na kukazia kuwa jina lake ni biashara.

Nahisi sio mara moja kunitaja kwenye nyimbo zake, Nakumbuka kuna wimbo hapo awali alinitaja. Mimi siwezi kumtaja hata kwenye meseji, Kwani nikitaja majina 10 ambayo nazungumza na watu sidhani kama jina lake ninaweza nikalikumbuka. Lakini yeye anavyoandika nyimbo zake analiona jina langu, Mimi ni biashara ni deal kubwa kwake,” amesema Bilnass.

Bilnass kabla ya majibu haya, Ali-Tweet kwenye mtandao wa Twitter kwa kumshambulia Nay wa Mitego na baadae akafuta Tweet hiyo, Hii ni baada ya wimbo wa Ipo Sawa kuachiwa.

Nay wa Mitego kwenye wimbo wake wa hivi karibu wa ‘Ipo Sawa’ alimtaja Bilnass kwenye baadhi ya mashairi ya wimbo huo alisikika akisema “Hivi unajua mzee baba?  Huku Nenga na Nandy wamerudisha mahaba Wamerudisha mahaba?  Madem bwana?“.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents