Technology

Binadamu kuishi milele kama jaribio la kuonganisha ubongo na mfumo wa kompyuta litakamilika (Video)

Je unatamani kuishi milele?. Huko nchini Marekani mjasiriamali mmoja wa masuala ya teknolojia, Eloni  Musk anadhanii binadamu huwenda wakaepuka kifo kutokana na ujio wa teknolojia mbalimbali duniani.

https://youtu.be/7WQ7OWZnZAs

Mwanasayansi huyo kwa sasa anashughulikia teknolojia ambayo itaunganisha mfumo wa ubongo wa binadamu na kompyuta hali ambayo itazuia miili ya binadamu kutozeeka na kufungua miingiliano na kidigitali daima.

Musk amedai mfumo huo utaweza kumsaidia binadamu kuishi bila kuzeeka na kuunganisha miili ya binadamu na mifumo ya kigitali.

Ubongo wa binadamu una nyaya 68 mtandao ambao unaweza kuunganisha mfumo wa ubongo wa binadamu na wakomputa.

Pia wamedai mfumo huo unaweza kuamisha akili za binadamu na kuzipeleka kwenye mfumo wa komputa lakini wadau wa mambo wamedai mfumo huo hauwezi kufanya kazi kwa kuwa ubongo wa binadamu una siri nyingi.

Mfumo huo ambao umepewa jina transhumanism, umeonekana kupingwa na wadau wengi wa sayansi kwa madai akili za binadamu haziwezi kuamishika.

Source: BBC

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents