Michezo

Bingwa wa dunia wa IBF, WBA na WBO, Anthony Joshua atakuwa na kibarua kizito leo mbele ya Povetkin

Bingwa wa dunia wa uzito wa juu, Anthony Joshua anatarajia kushuka kwenye uwanja wa Wembley kuzipiga na Alexander Povetkin hii leo siku ya Jumamosi.

Joshua raia wa Uingereza atashuka ulingoni kuitetea mikanda yake ya dhahabu ya IBF, WBA na WBO dhidi ya mpinzani wake Povetkin ambaye atuwa katika jiji la London akiwa na utimamu wa mwili na kiakili huku akiwa na lengo moja tu kumshinda mpinzani wake.

Anthony Joshua

Kuelekea pambano hilo Joshua amesema kuwa wote wamejaaliwa kuwa na ujuzi wa hali ya juu pamoja na tekniki za kupambana hivyo akiamini kuwa aliyekuwa bora ndiye atakaye ibuka na shujaa ulingoni.

Alexander Povetkin

Wakati kwa upande wake, Povetkin amemwagia sifa lukuki mpinzani wake, AJ kwakusema kuwa yupo imara hasa katika watu wenye level ya uzito wake na kuwa mwingi wa furaha kupata nafasi hiyo ambayo anaamini atawapatia pambano zuri mashabiki watakao hudhuria ulingoni hii leo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents