Michezo

Bingwa wa La liga nchini Hispania kujulikana leo

Mbio za kuwania Ubingwa wa ligi kuu ya nchini Hispania maarufu kama Laliga utaamuliwa hapo kesho siku ya Jumapili baada ya michezo kadhaa kuchezwa.


Klabu ya Real Madrid mara ya mwisho kuchukua Ubingwa wa La Liga mwaka 2012

Vinara wa Ligi hiyo klabu ya Real Madrid wana uchu wakunyakuwa kombe hilo baada ya kulikosa kwa Misimu mitano, na hivyo kuwa na kibarua kizito cha kuizuia klabu ya Barcelona kuchukua tena kwa msimu wa tatu mfululizo.

Wakati wapinzani wa Real Madrid wa kombe la klabu bingwa Barani Ulaya {UEFA}, klabu ya Juventus wao walifanikiwa kuchukua kombe la Serie A kwa mara ya sita mfululizo mwishoni mwa juma lililopita na sasa wakisubiria kombe la klabu bingwa UEFA pekee.

Kocha raia wa Ureno, Jose Mourinho, ndie aliewezesha klabu ya Real Madrid kutwaa kombe la Hispania kwa mara ya mwisho mwaka 2012 na baada ya hapo mpaka hivi sasa klabu hiyo haijafanikiwa kunyakuwa tena taji hilo la La liga.

Klabu ya Barcelona imechukua taji hilo la La Liga, mara tatu wakati klabu ya Atletico Madrid wakichukua ubingwa huo mwaka 2014.
Bado mashabiki wa Real wanasubiria ushindi katika mchezo wa mwisho dhdi ya Malaga, ili waweze kusherehekea ubingwa .

Kwa upande wa kikosi cha kocha, Zinedine Zidane’s kinahitaji alama ili kuizidi klabu ya Barcelona, ambao nao watakuwa na kibarua jumapili, wakiwa wana cheza na klabu ya ,Eibar , wakihitaji ushindi, baada ya kushinda katika mchezo wao wa mwisho katikati ya wiki kwa jumla ya magoli 4 kwa 1 dhidi ya Celta Vigo.

Kama Real itapoteza ubingwa hii itakuwa ni kwa mara ya kwanza kwa kocha wa Real madrid, Zidane tangu awaongoze vijana hawa wa Bernabeu akiwa katika msimu mzima klabu hapo.

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents