Michezo

Bingwa wa masumbwi wa dunia, LaMotta afariki

Bingwa wa zamani wadunia wa Marekani wa uzito wa kati na mchekeshaji, Jake LaMotta amefariki dunia Septemba 19 mwaka huu akiwa na umri wa 95.

 

LaMotta ambaye alitamba zaidi katika tasnia ya mchezo wa ngumi kuanzia miaka ya 1949 hadi 1951 amefariki nyumbani kwake kutokana na tatizo la homa ya mapafu.

Kifo cha bingwa huyo wa uzito wa kati wa Marekani, Giacobbe LaMotta kilitangazwa kupitia  mtandao wa kijamii na mtoto wake  mkubwa wa kike ambaye bondia huyo alizaa na mke wake wa pili mwanamitindo Vikki LaMotta.

LaMotta  ambaye ni mzaliwa wa July 10 mwaka 1922 atakumbukwa kwa uvaaji wa kaptula yenye mistari ya chuichui na wakati fulani alikua akiingiza uchekeshaji wakati akipigana jambo lililomfanya mpinzani wake kuishia kucheka na yeye kushinda.

Mke wa marehemu LaMotta, ambaye ni Denise Baker amesema kuwa “Nahitaji watu wafahamu kuwa alikuwa shujaa, mwenye busara, mwenye nguvu”.

LaMotta ni bingwa wa dunia wa uzito wakati June  mwaka 1949  wakati alipokabiliana na mfaransa, Marcel Cerdan na kumpiga katika raundi ya 10 ya pambano.

Bingwa huyo wazamani amepambana  jumla ya mapambano 106 katika miaka 13 ya tasnia yake ya ngumi, akishinda mara 83 akitoa suluhu mara 4 na kupigwa mapambano 19 huku katika maisha yake ya kawaida akiwa ameowa mara saba akiwa na jumla ya watoto wakike wanne na wakiume wawili wakati mtoto wake wakwanza wakiume, Jake LaMotta Jr amefariki kutokana na tatizo la saratani ya Ini February  mwaka 1998.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents