Michezo

Bingwa wa Wimbledon, Jana Novotna afariki dunia

Mchezaji tenis wa zamani wa Jamuhuri  ya Czech,  Jana Novotna amefariki dunia siku ya Jumapili ya wikiendi hii kufuatia kuugua ugonjwa wa kansa.

Bingwa huyo wa zamani wa Wimbledon, Novotna amefariki akiwa na umri wa miaka 49, wadau wa tenis humkumbuka zaidi pale alipomwaga machozi hadharani baada ya kukosa kutwaa taji hilo mwaka 1993 na 1997 kabla ya kushinda michuano ya Grand Slam mwaka 1998 kwa kumfunga mwanadada Nathalie Tauziat.

Chama cha tenis cha wanawake duniani (WTA) kimesema kuwa Novotna, ambaye amefariki kwa ugonjwa wa kansa kifochake kilikuwa katika hali ya utulivu na amani huku akiwa amezungukwa na familia yake.

“Jana alikuwa akiwavutia watu wengi ndani na nje ya mchezo kwa mtu yeyote aliyewahi kupata nafasi ya kumfahamu.” Alisema mtendaji mkuu wa WTA.

“Nyota yake siku zote itaangaza katika historia ya WTA. Tunaungana na familia ya marehemu katika kipindi hiki kigumu.”

Novotna ameshinda jumla ya mataji 17 ya Grand Slam katika kipindi chake chote alichokuwa akicheza mchezo huo, huku akitwaa medali tatu za Olympic.

Novotna ameanza kuingia katika mchezo wa tenis wa kulipwa mwaka 1987  na kufanya vizuri hali iliyopelekea wapenzi wa mchezo huo kumfuatilia huku akifanikiwa kujenga jina lake mwaka 1990 miaka nane kabla ya kutwaa ubingwa wa Wimbledon.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents