Habari

Binti aliyebakwa na rafiki wa baba yake mzazi aomba aruhusiwe kutoa mimba

Wazazi wa Msichana wa miaka 13 aliyebakwa na rafiki wa karibu wa baba yake mzazi huko nchini India wameenda mahakamani kuomba msaada wa kisheria ili mtoto wao aendelee na masomo.

India is home to 400 million children

Msichana huyo ambaye wazazi wake walimpeleka hospitali moja jijini Mumbai nchini India kupata vipimo vya afya baada ya kuona mtoto wao anaongezeka unene kila siku walipewa taarifa na Daktari kuwa tayari mtoto wao anaujauzito wa wiki 20.

Dr Nikhil Datar aliyempima mtoto huyo amesema wazazi wake walikuwa hawajui chochote kuhusu mtoto wao na hata alipowaambia kuwa ni mjamzito hawakuamini kwa mara ya kwanza ndipo ikamfanya arudie tena vipimo.

“Walimleta mtoto wao kwa matibabu tarehe 9 agosti mwaka huu baada ya kuona mtoto wao anaongezeka unene kila siku na ndipo nikamfanyia vipimo na kubaini kuwa alikuwa na ujauzito wa wiki 20 ingawaje hawakuamini kwa mara ya kwanza nilipowapa taarifa”,amesema Dr Nikhil Datar kwenye mahojiano yake na mtandao wa Shirika la kusaidia watoto Ulimwenguni UNICEF.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwenye mtandao wa BBC zinasema kuwa wazazi wa mtoto huyo tayari wameenda mahakamani kufuatilia masuala ya kisheria kuangalia kama kuna uwezekano wa mtoto huyo anawezakutoa mimba hiyo.

Maelezo kutoka kwa Baba mzazi wa mtoto huyo aliyebakwa na swahiba wake, amedai kuwa kwa sasa anachoshughulikia ni kuhahakisha mtoto wake anarejea kwenye hali ya kawaida.

Hata hivyo kwa mijibu wa sheria za India huenda mtoto huyo akakosa ruhusa ya kutoa mimba hiyo kwani sheria naruhusu kutoa mimba kwa yule mjamzito anayepatwa na matatizo ya ujauzito wa kuanzia wiki 30.

SOMA ZAIDI- Baraza la kijiji laamuru dada wa kaka aliyebaka abakwe (+Video)

Kwa mujibu wa Shirika la Watoto Ulimwenguni (UNICEF), nchini India mtoto mmoja mwenye miaka (16) hubakwa kila baada ya masaa mawili, na kila baada ya masaa 10 mtoto aliyechini ya miaka 10 hufanyiwa pia vitendo hivyo vya kikatili.

Kwa mwaka 2015 pekee India imeripotiwa kuwa na kesi 10,00 za ubakaji wa watoto waliochini ya umri wa miaka 16.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents