Uncategorized

Binti Komando atambulisha rasmi kipindi chake cha 'Diary ya Lady Jaydee'

Lady Jaydee akiongea na waandishi wa habari

Msanii nguli wa kike ambaye ana majina mengi kama Komando, Jide, Mama Some food n. k leo asubuhi ameongea na waandishi wa habari na kutoa taarifa rasmi kwenda kwa watanzania juu ya ujio wa kipindi chake kipya cha TV kitakachoitwa “Diary ya Lady Jaydee”.

Msanii huyo wa kike ambaye kwa sasa anatamba kwa hit song yake ya ya “ Mimi Ni Mimi” alisema kipindi hicho cha Diary ya Lady Jaydee kitazungumzia maisha yake kwa undani kikitazama mambo kama njia aliyopitia kufanikiwa, mahusuiano yake binafsi na mwandani wake pamoja na washkaji,wadau na ndugu jamaa na marafiki, ikiangalia pia namna alivyoweza na anavyokabiliana changamoto mbali mbali, mipango yake ya kimuziki, maisha na biashara.

Naye mkuu wa vipindi katika kituo cha televisheni cha East Africa TV Lidya Igarabuza alisema katika kipindi hicho kitakachokuwa kikiruka siku ya kila Jumapili ya wikiendi hii na kuendelea kitakuwa kikionekana kuanzia mida ya saa 3 usiku na kuonekana kwa nusu saa tu.

Mkuu wa vipindi EATV Lidya akifafanua jambo huku Lady Jaydee akifuatilia kwa makini
Lady Jaydee akifurahia jambo na waandishi wa habari baada ya kumtania kidogo

Akiendelea Lidya alisema wao kama kituo namba moja cha TV kwa vijana wamechukua fursa ya kukubali kuonyesha kipindi hicho cha Diary ya Lady Jaydee kwa sababu Jaydee msanii mkubwa tu Tanzania bali Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla na hivyo kwa sababu ana mashabiki wengi ni faraja kubwa kwa kituo hicho kuongeza idadi ya watazamaji ambao ni wapenzi wa msanii huyo.

Akimalizia mkuu huyo wa vipindi alisema kipindi hicho kitakuwa na episode 52 kwa maana kipindi kimoja kwa wiki kwa mwaka mzima hivyo kuwataka watazamaji wa TV hiyo kukaa mkao wa kula wakisubiri kuona ni nini kitaonekana kuanzia jumapili hii.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents