Habari

Binti mdogo akili kubwa, atoa fursa kwa vijana 250 Dar (Picha)

Jumapili hii vijana zaidi ya 250 wamepata mafunzo ya Interion Design kupitia semina iliyoandaliwa na mjasiriamali kijana Anezylitta. Semina hiyo ambayo iliendeshwa kwa vitendo zaidi ilifanyika City Mall jijini Dar es salaam.


Anezy akizungumza na vijana waliojitokeza.

Vijana hao wote walipewa vyeti baada ya kushiriki mafunzo hayo ili na wao waanze kujitegemea katika sekta hiyo ya mapambo.

Akiongea na waandishi muda mchache baada ya kumaliza mafunzo hayo, Anezy alisema alianzisha mafunzo hayo ili kutoa fursa kwa vijana ambao wanapenda kufanya ‘Interion Design’ na wanashindwa kujua waanzie wapi.

Mkufunzi akitema madini

“Mimi nafanya Interion Design kwa miaka mingi sasa na tayari na duka langu la vifaa mbalimbali hapa City Mall haya ni mafanikio ambayo nilipenda kushare na vijana wenzangu,” alisema Anezy “Kwa sababu vijana wengi ninaokutana nao wanatamani kuwa kama mimi, wengine wanataka kuwa mafundi wa kubandika wallpaper, nikaona bora niandae semina ambayo nitawapatia vijana mafunzo ambayo yatawafanya kuwa wajasiriamali,”

Aliongeza “Pia nimewambia material ya kazi inayo, duka langu lina kila kitu kwaajili ya Interion Design, wewe kwa sababu ni fundi mpya, ukimpata mteja njoo naye mnunue material mimi nitakupa fundi wangu mzoefu kama utahitaji wa kwenda kufanya naye kazi ili kukuongezea ujuzi zaidi. Lakini wale mafundi wataokuwa wanaleta wateja kuna kamesheni yao, lakini kama vilivyosema haya mafunzo na kuwajengea uwezo katika hizi kazi za Interion Design,”

Kwa upande wa vijana ambao walibahatika kupata mafunzo hayo walisema mafunzo hayo yatawajengea uwezo wa kufanya kazi kwa kijiamini.

“Kusema kweli haya mafunzo ni mazuri sana, sasa hivi hata mimi naweza kuingia mtaani za kuanza kutafuta kazi za Interion Design na kama ulivyomsikia Anezy kama tukikwama milango yao ipo wazi kwaajili ya kutusaidia, hii ni fursa kwetu tunamshukuru sana” alisema Hemed.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents