Habari

Binti Mnigeria Zuriel Oduwole (11) achaguliwa na Mama Salma Kikwete kuwa balozi wa WAMA

Binti mwenye miaka 11 mwenye asili ya Nigeria aliyeweka historia mwaka kuu kwa kuwa mtu mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kuhojiwa na kutokea katika jarida la Forbes toleo la August, Zuriel Oduwole na ambaye hivi karibuni aliitembelea Tanzania, amechaguliwa na Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete kuwa balozi wa Taasisi yake ya Wanawake na Maendeleo, WAMA.

Zuriel

Ujio wa Zuriel nchini Tanzania ulikuwa sehemu ya ziara yake ya Afrika Mashariki katika uzinduzi wa program yake ya Dream Up, Speak Up, Stand Up yenye lengo la kuwahamasisha wasichana wa kiafrica.

Zuriel & Salma Kikwete1
Zuriel akiwa na mama Salma Kikwete

October 11 Zuriel alihudhuria tukio lililoandaliwa na Umoja wa Mataifa UNFPA Dar es salaam ambalo lililenga kupunguza ndoa za utotoni kwa Tanzania.

Zuriel & Salma Kikwete2

Binti huyo ambaye makazi yake ni California, Marekani kwa sasa pia alialikwa Mama Salma Kikwete kumtembelea. Katika mwaliko huo Mama Salma alimsifia Zuriel kwa kuhamasisha maswala ya elimu kwa watoto wa kike kwa viongozi wa nchi mbalimbali za Afrika na kumchagua kuwa balozi wa WAMA.

Ingia hapa kumfahamu zaidi Zuriel Oduwole.

Source: informationng.com Picha: Full Shangwe Blog

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents