AFCON 2019 Tupogo!
Vodacom Data Datani!

Binti wa miaka 17 amponza Drake, wadau wataka ashtakiwe kwa kosa la unyanyasaji kingono(+video)

Msanii wa muziki kutoka Canada, Drake huenda akapatwa na majanga ya kuburuzwa mahakamani kwa kosa la kumtomasa binti wa miaka 17 jukwaani.

Drake alifanya tukio hilo mwaka 2010 kwenye show yake mjini Colorado Marekani, ambapo alimuita msichana huyo jukwaani na kuanza kumuuliza maswali huku akimtomasa kifuani.

Wanaharakati wameibua kashfa hiyo ya kutaka Drake akamatwe, ikiwa bado kuna vugu vugu la sakata la unyanyasaji wa kingono linalomkabili R. Kelly.

Soma zaidi – Wanawake walionyanyaswa kingono na R. Kelly wafunguka mazito ‘alituvua nguo na kuanza kutu..’ 

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW