Habari

Birthday ya EATV na East African Radio ilikuwa poa

EATVHatimae lile tamasha la kuadhimisha miaka mitano ya kituo cha runinga cha EATV Channel 5 na East African Radio, lilifanikiwa na kufana ile mbaya kama ilivyokuwa likitangazwa

AY na Prezzo


Hatimae lile tamasha la kuadhimisha miaka mitano ya kituo cha runinga cha EATV Channel 5 na East African Radio, lilifanikiwa na kufana ile mbaya kama ilivyokuwa likitangazwa ambapo nyuso za furaha zilionekana kwa kila mpenzi wa burudani aliyehudhuria viwanjani hapo, ama kweli Birthday ilinoga ile mbaya.


Wasanii kutoka nchi jirani kama vile Kenya na Uganda wakishirikiana na wasanii wa hapa nchini waliweza kufanya makamuzi ya ukweli na kuiadhimisha kikamilifu miaka mitano ya ya vituo hivyo vya burudani hapa nchini.


“ukweli ni kwamba wasanii kutoka nchi jirani wamewafunika wasanii wetu wa kibongo ile kinoma kwani inaonekana kuwa wenzetu wamejiandaa kwa ajili onyesho, hebu cheki msanii kama DNA yaani yuko peke yake lakini utadhani wako kumi jukwaani, Hao kina dada wa kundi la blu 3 ni sooo mtu wangu wamekamua bovu, tatizo la wabongo kila siku wanafanya kitu kile kile hata muonekano wao katika show hauna mvuto ka wenzetu” alisema mmoja wa mashabiki waliohudhuria katika tamasha hilo aliyejulikana kwa jina la Richard.


Kila kizuri hakikosi kasoro ila kibongo bongo Show ya One Mic ilikuwa bomba sana kwani ni nadra sana kuwakusanya wasanii wakali kama wale katika onesho moja.


Upande wa watanzania msanii Ambwene Yesaya a.k.a AY aliweza kufanya show ambayo watanzania wengi hawakuitarajia kutokana na kutoonekana jukwaani kwa muda mrefu sana “Dah huyu mchizi kweli yuko gado na kujichanganya kwake na wasanii wa nchi kama Kenya na Uganda kumemsaidia sana kijana kuwa fiti” alisema mwanadada mmoja ambaye alionekana kushangilia sana hasa msanii huyu alipokuwa jukwaani ambaye hakutaka jina lake litajwe.


Lakini kwa ujumla wasanii wote walifanya show nzuri japo kuonekana kwa mapungufu hilo ni kawaida kama yameshindikana kurekebishwa kwenye Birthday hii basi yatakuwa poa birthday nyingine.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents