Burudani

Bishanga kurejea kwenye TV na series za mbio za magari

Muigizaji mkongwe wa runinga ambaye kwa sasa hayupo tena kwenye kazi hiyo, Raymond Allen maarufu kama Bishanga, amesema anatarajia kurejea tena kwenye TV lakini katika tamthilia tofauti.

11324473_897101610336440_1420907235_n
Bishanga na partner wake kwenye red carpet ya tuzo za watu, May 22

Akiongea na Bongo5, Bishanga ambaye kwa sasa anafanya kazi kwenye kampuni ya ujenzi, amesema mpango wake ni kuja na kipindi cha TV cha magari.

“Nitarudi lakini kwa style tofauti kabisa,” Bishanga ameiambia Bongo5. “Mimi napenda sana racing (mbio za magari), lakini kwa mtazamo mwingine, si kwa kushindana na mtu mwingine. Mtu aone ninavyoweza kucheza na gari na nini. That’s what I want to put on art,” alisisitiza.

“Itakuwa kama soap opera ambayo itakuwa in one of the television stations.”

Amesema amekwisha anza kuifanyia kazi lakini bado anahitaji nguvu zaidi kuifanikisha. “Naitengenezea na nimeiandikia, kuna mtu ananisaidia kuiandikia script, nafikiri itakuwa vizuri.”

Bishanga alijipatia umaarufu mkubwa kupitia tamthilia ya Mambo Hayo aliyokuwa akiigiza pamoja na Rich, Waridi na Aisha.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents