Bizzman ajitupa BBC

BizzmanMsanii nyota Bizman, amekata utepe kwa wasanii wa Tanzania kuingia katika shindano la wimbo bora wa BBC, lililoanza Julai Mosi mwaka huu.

BizzmanMsanii nyota Bizman, amekata utepe kwa wasanii wa Tanzania kuingia katika shindano la wimbo bora wa BBC, lililoanza Julai Mosi mwaka huu.

Bizman, anayesifika na vibao kadhaa vya kusisimua jana ametupa karata yake katika studio za Idhaa ya Kiswahili ya BBC London kwa kuwasilisha kibao kipya kinachokwenda kwa
mahadhi ya kizazi kipya.

Kwa mujibu wa matangazo ya BBC yaliyosikika jana, Bizman amekuwa msanii wa kwanza wa Kitanzania nyota kuwasilisha wimbo wake katika shindano hilo ambalo bingwa atajipatia
zawadi nono zitakazowekwa hadharani wakati wowote.

Hata hivyo, jina la wimbo huo halikutajwa ingawa Bizman anasikika akiimba kwa kusaidiana na msanii mwingine mwenye sauti nyororo katika kunogesha wimbo huo na hatimaye kuibuka mshindi.

BBC imekuwa ikiendesha shindano hilo kwa zaidi ya wiki tatu sasa ikiwashirikisha wasikilizaji wake kote duniani hususan wanaojua lugha ya Kiswahili inayopigania kuchukua nafasi ulimwenguni.

 

{mos_sb_discuss:6}

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW