Burudani

Blac Chyna atemana na mpenzi wake mpya

Video vixer wa dunia, Blac Chyna ametemana na kijana Mechie alikuwa mpenzi wake mpya baada ya kutemana na mzazi mwenzake Rob Kardashian.

Blac ameamua kutemana na mpenzi wake baada ya kuona kuwa amekuwa akitaniana sana na wanawake katika mitandao ya kijamii, kitendo ambacho kimekuwa kinamkera mrembo huyo, ndipo akaamua kumtolea uvivu na kumtaka kila mtu aendelee na maisha yake.

Wawili hao wamekuwa katika mahusiano yasiyozidi miezi miwili, hata hiyo kijana huyo baada ya kuona hali imeharibika ameamua kufuta tatoo zilizokuwa na jina la mpenzi wake huyo.

Inadaiwa kuwa moja ya chanzo cha wawili hao kuachani ni baada ya ni picha iliyosambaa ikimuonyesha Blac na Tristan Thompson pamoja, huku tetesi zikidai kuwa wana-date ili walipize kisas kwa familia ya Kardashian.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents