BurudaniUncategorized

Black Panther yavunja rekodi box office, yaingiza bilioni 432 kwa siku tatu

Matarajio ya filamu ya ‘Black Panther’ kufanya vizuri yameanza kuonekana katika siku tatu tangu ilipoachiwa Ijumaa iliyopita mjini Johannesburg, Afrika Kusini.

Filamu hiyo imetajwa kuingiza kiasi cha dola milioni 192 ambapo kwa fedha za kitanzania ni zaidi ya shilingi bilioni 432 kwa nchini Marekani.

Kutokana na kiasi hicho kilichoingiza filamu hiyo, kimevunja rekodi zilizowahi kuwekwa na filamu kibao kwenye box office, ikiwemo ile iliyowahi kuwekwa April mwaka jana na The Fate of the Furious, iliyoongozwa na Felix Gary Gray.

Wakati huo huo kampuni ya The Walt Disney Company yenye makao yake makuu mjini California, Marekani, inakadiria kuwa Black Panther itaingiza kiasi cha dola milioni 218 ndani ya siku nne kwa Marekani pekee.

Filamu hiyo pia imeingiza kiasi cha dola milioni 361 kutoka sehemu zingine duniani. Pia Black Panther imekuwa filamu ya pili kutoka kwenye kampuni ya Marvel kuwa na ufunguzi mkubwa zaidi ikiongozwa na filamu ya The Avengers ya mwaka 2012.

Black Panther imewakutanisha waigizaji kama Chadwick Boseman ambaye ndio staa wa filamu hiyo, Lupita Nyong’o, Michael B. Jordan, Danai Gurira, John Kani na Connie Chiume.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents