Michezo

BMT yatangaza uchaguzi mkuu TBF

Baraza la mchezo la Taifa (BMT) limetangaza uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa kikapu Tanzania (TBF) unaotarajiwa kufanyika tarehe 29 hadi 30 mwezi Disemba, 2017 Mkoani Dodoma.

Fomu zitaanza kutolewa katika Ofisi za Baraza kuanzia tarehe 16 mwezi Novemba hadi 22 mwezi Disemba mwaka 2017.

Aidha,tarehe ya usaili na ukumbi utakaotumika kwa zoezi zima la uchaguzi tutawataarifu hapo baadae.

Nafasi zinazogombewa ni;

1) Rais

2) Makamu wa Rais

3) Katibu Mkuu

4) Katibu mkuu msaidizi

5) Mweka Hazina Ada ya fomu kwa nafasi hizi ni sh. 150,000,

6) Nafasi nane (8) za kamisheni :-

  1. Kamisheni ya makocha
  2. Kamisheni ya waamuzi
  3. Kamisheni ya watoto wadogo na maendeleo ya mashule
  4. Kamisheni ya wanawake
  5. Kamisheni ya mipango na maendeleo
  6. Kamisheni ya watu wenye ulemavu
  7. Kamisheni ya Tiba ya wanamichezo
  8. Kamisheni ya ufuncii na uendeshaji wa mashindano.

Ada ya fomu kwa nafasi hizi ni sh. 100,000/=

Baraza linatoa wito kwa wenye sifa na wenye nia njema ya kuuendeleza mchezo huu nchini kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu wapiga kura wafanye maamuzi sahihi kwa maendeleo ya mchezo wa mpira wa kikapu nchini.

Malipo ya fomu yafanyike katika Akaunti ya Baraza kwa jina la National

Sports Council A. N. 20401100013-Bank ya NMB na kuwasilishwa Baraza fomu iliyojazwa pamoja na risiti iliyolipiwa Benki.

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents