Tupo Nawe

Bob Junior aeleza sababu iliyomfanya aendelee kuwa kimya kwa muda mrefu

Mtayarishaji wa muziki wa Sharobaro Records na muimbaji wa nyimbo, Bob Junior amesema moja ya sababu za ukimya wake ni kutoridhishwa na nyimbo zake mwenyewe anazorekodi.

Bob Junior

Bob junior amesema kila anaposikiliza ngoma alizorekodi anahisi hazifai kutoka kwasababu anaamini mashabiki wanahitaji kitu kipya.

Akizungumza na Planet Bongo ya East Afrika Radio, amesema anajua mashabiki wanamuitaji Bob Junior mpya na si kama waliyemzoea lakini akisikiliza ngoma alizorekodi anaona bado zina ladha ya bob junior wa zamani.

Hata hivyo aametoa ahadi kuwa mashabiki wake wakae tayari kwa ngoma yake mpya mwishoni mwa mwezi huu (January)au mwanzoni mwa mwezi ujao (February).

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW